Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameahidi kuwa kama CCM itachaguliwa kuendelea kuongoza nchi, wataendelea kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi katika Jimbo la Nzega Vijijini, ikiwemo ujenzi wa vituo vipya vya afya viwili na zahanati kumi, ili kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Ndala, Dkt. Nchimbi amesema serikali itahakikisha sekta ya mifugo inaimarika kwa kujenga majosho mapya ya kuoshea mifugo na machinjio ya kisasa katika minada minne mikubwa ya wilaya hiyo, hatua itakayoongeza thamani ya mazao ya mifugo na kuinua kipato cha wafugaji.

Ameongeza kuwa serikali kupitia Ilani ya CCM imeweka mkakati wa kuwapa kipaumbele wachimbaji wadogo, huku tafiti za maeneo mapya ya madini zikiendelea na utoaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo ukiimarishwa, ili kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa tija na kwa kufuata sheria.

✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *