Mgombea ubunge wa Jimbo la Nzega Vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Neto Kapalata, ameahidi kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kuhakikisha Ndala inakuwa mji mdogo wa kisasa wa kibiashara utakaokuza uchumi wa wananchi wa Nzega Vijijini.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi katika kata ya Nata Oktoba 4, 2025, Kapalata amesema Ilani ya CCM katika eneo hilo imeelekeza ujenzi wa machinjio ya kisasa na uboreshejwaji wa barabara kwa kiwango cha changarawe ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa.
Ameomba pia kuanzishwa kwa taasisi za kibenki na kituo cha polisi katika eneo la Ndala ili kuweka mazingira salama na rafiki kwa biashara kustawi.
✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates