Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), Irene Mlola amesema Tanzania imeshika nafasi ya pili duniani kwa uzalishaji wa mbaazi, huku msimu wa mwaka jana ikisafirisha takriban tani 350,000 kwenda India.

Kwa mujibu wa Mlola, amesema kwa msimu wa mwaka huu, uzalishaji wa mbaazi nchini unatarajiwa kuzidi tani 400,000, ongezeko linalotarajiwa kuongeza faida kwa wakulima wa zao hilo. Hata hivyo, ongezeko hili la uzalishaji limechangia kushuka kwa bei ya mbaazi katika masoko ya kimataifa.

Amesema kutokana na hali hiyo na ili kuwawezesha wakulima kupata soko la uhakika, Serikali ya Tanzania inachukua hatua za makusudi, ikiwa ni pamoja na Mpango wa kuuza mbaazi moja kwa moja kwa Serikali ya India.

COPRA imeongoza ujumbe wa Serikali kwenda India kwa lengo la kuendeleza mazungumzo, ambapo wamekutana na Katibu Mkuu wa wizara inayosimamia masuala ya walaji.

Mkutano huo umejadili Mpango wa Tanzania wa kuuza mbaazi na hatua za utekelezaji wake.

✍ John Kasembe
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *