Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amevipongeza vikundi vya wajasiriamali wa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam waliopokea mikopo ya pikipiki na bajaji zilizotokana na mikopo ya asilimia 10 ya vijana, wanawake na wazee inayotolewa na halmashauri zote nchini.

Sambamba na hilo amewataka wanufaika hao kueleza kwa ukweli na uwazi kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii mafanikio ambayo yanapatikana nchini kupitia Serikali ya Awamu ya Sita badala ya ku-post taarifa ambazo zinahamasisha vurugu na zinazoegemea upande mmoja bila kuonesha uhalisia wa namna jamii inavyonufaika na kupiga hatua.

Imeandaliwa na @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *