
Marekani ilitangaza Ijumaa, siku ya Oktoba 3, kwamba ilishambulia meli nyingine kutoka Venezuela. Kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Wafanyabiashara wanne madawa ya kulevya ndo walikuwa ndani ya meli hiyo. Hiki ni kipindi kipya katika mvutano unaoongezeka kati ya nchi hizo mbili.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa Caracas, Alice Campaignolle
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth alitangaza kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X wameharibu meli nyingine ya Zodiac kutoka Venezuela siku ya Ijumaa, Oktoba 3.
Ni mwezi mmoja tangu meli za Kimarekani zipelekwe kwenye Bahari ya Caribbean kwenye pwani ya Venezuela ili “kupambana na ulanguzi wa dawa za kulevya,” kkulingana na maneno ya Rais Donald Trump. Jumla ya meli tano zimeripotiwa kuharibiwa tangu wakati huo, na kusababisha vifo vya angalau watu 21.
Caracas ilishutumu oparesheni hizi, ikizitaja kuwa ni mauaji yasiyo ya haki, na kumtaka mkuu wa Pentagon kuachana na “msimamo wake wa kizembe na wa kivita, ambao unawakilisha tishio kwa amani na utulivu katika eneo hilo.”
Siku iliyotangulia, Alhamisi, Waziri wa Ulinzi wa Venezuela aliripoti kupaa kwa ndege za kivita za Marekani karibu sana na anga ya nchi hiyo. “Uchochezi,” kwa maneno yake.
Mvutano unaendelea kuongezeka kati ya Washington na Caracas. Na kwa upande wa Venezuela, mazoezi ya kijeshi na ya kiraia yalifanyika Oktoba 4 ili kuboresha “utaratibu wa ulinzi wa eneo.”