Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Warioba amewataka Watanzania kuungana na kauli ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kupinga vikali juhudi za kulihusisha jeshi hilo na siasa.

Akizungumza leo mkoani Mara, Mzee Butiku amesema Jeshi la Tanzania ni chombo cha kitaifa kinachoongozwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na si sehemu ya majibizano ya kisiasa.

Ameonya wananchi kupuuza taarifa zisizo rasmi hasa wakati wa uchaguzi, akisisitiza umuhimu wa kulinda Katiba, amani na heshima ya vyombo vya ulinzi na usalama.

✍ Augustine Mgendi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *