
Siku ya Alhamisi, Putin alisema Ukraine haiwezi kutumia makombora hayo bila ushiriki wa moja kwa moja wa wanajeshi la Marekani akionya kuwa usambazaji wowote wa makombora hayo utachukuliwa kama hatua ya kuuchochea mzozo huo.
Viongozi hao wawili wamekuwa wakirushiana maneno katika siku za hivi karibuni ambapo Trump alimuita Putin kuwa “chui wa karatasi” kwa kushindwa kumaliza vita Ukraine, huku Putin akisema kuwa NATO ndio wanaopaswa kuitwa hivo kwa kushindwa kuzuia mafanikio yake katika uwanja wa vita. Hayo yakiarifiwa, vita vinaendelea ambapo watu watano wameripotiwa kuuawa nchini Ukraine kufuatia mashambulizi ya makombora na droni ya Urusi.