
Mke wa rais wa zamani Simone Ehivet, ambaye anagombea katika uchaguzi wa Oktoba 25, amepata uungwaji mkono kutoka ndani ya upinzani: ule wa waziri wa zamani Charles Blé Goudé, ambaye alitoa tangazo hilo siku ya Jumamosi, Oktoba 4, wakati wa kongamano lisilo la kawaida la chama chake, Cojep, katika mji mkuu, Yamoussoukro. Aliondolewa kwenye orodha ya wapiga kura kufuatia kutiwa hatiani na mahakama za Côte d’Ivoire, Charles Blé Goudé hakuwasilisha faili ya uchaguzi wa mwaka huu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Abidjan, Bineta Diagne
Nchini Côte d’Ivoire, karibu wanaharakati 200 walikusanyika kwa kongamano siku ya Jumamosi hii, Oktoba 4 huko Yamoussoukro, walipiga kura kwa wingi kwa Cojep kumuunga mkono Simone Ehivet, mke wa zamani wa Laurent Gbagbo. Kwa sababu kiongozi wao, Charles Blé Goudé, aliondolewa kwenye orodha ya wapiga kura kutokana na kutiwa hatiani na mahakama za Côte d’Ivoire. Kwa hiyo yuko nje ya kinyang’anyiro cha uchaguzi huu. Mnamo mwezi Septemba 2023, chama chake kilikuwa tayari kimechagua kutoshiriki katika uchaguzi wa wa viongozi wa manispaa na mikoa.
Baada ya kuonyesha mashaka kuhusu orodha ya wapiga kura, Charles Blé Goudé aliwaomba wanaharakati kuhamasishwa wakati huu ili kupiga kura. “Kuanzia kesho, nitarejea kumfanyia kampeni Simone Ehivet. Kulikuwa na uchaguzi hapa mnamo mwaka 2018, huko Plateau. Ehouo Jacques, ambaye sasa ni mbunge meya wa Plateau, anaongoza kwenye orodha hii ya wapiga kura. Ni kweli yeye hakamiliki. Lakini kwa orodha hii ya wapiga kura, Ehouo Jacques alichaguliwa? watu wale alitumia njia ya demokrasia na mimi ninawaangalia, ninawaambieni. kura milioni tano ziko huko.”
Kama Simone Ehivet, Charles Blé Goudé ameamua kusitisha ushiriki wake katika Muungano wa Mabadiliko ya Amani nchini Côte d’Ivoire. CAP CI iliundwa karibu mwaka mmoja uliopita, haswa ili kupata mazungumzo na viongozi ili kujelea upya mchakato wa uchaguzi.