Wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani wamefanya mazungumzo mjini Kabul kuhusu kufanikisha utaratibu wa safari za kawaida za kuwarejesha wahalifu wa Kiafghanistan. Mazungumzo hayo yalielezewa kama “majadiliano ya kitaalamu.” Kituo cha utangazaji cha umma cha Ujerumani, ARD kiliripoti kuwa afisa mwandamizi wa wizara hiyo alikuwa Kabul Jumatano iliyopita kujadili urejeshaji wa raia wa Afghanistan wenye rekodi ya uhalifu.Mawasiliano ya Ujerumani na Taliban ni suala lenye utata,kwa kuwa Ujerumani haina uhusiano rasmi wa kidiplomasia na kundi hilo, ambalo lilirudi madarakani Agosti 2021 na limewekwa pembeni kimataifa kutokana na ukiukaji wa haki za binadamu, hasa dhidi ya wanawake.Tangu Taliban ichukue mamlaka, Ujerumani imeyarejesha makundi ya raia wa Afghanistan mara mbili, kwa msaada wa Qatar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *