#HABARI: Hali ya mvutano imetokea baina ya mawakili wa Jamhuri na baadhi ya mawakili wa upande wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu pamoja wafuasi wa Chadema wakigombea sehemu ya kukaa katika ukumbi wa Mahakama kuu baada ya Jaji kutoa mapumziko ya dakika 30, ndipo imetokea hali hiyo ya yakutoelewana na kuanza kutupiana maneno.
Ndani ya ukumbi huo leo ni tofauti na siku nyengine ambazo kesi hiyo imekua ikiendelea ambapo wafuasi na wafuatiliaji ni wachache, wengi wakiwa ni mawakili wa Jamhuri na waupande wa Lissu na baadhi ya maofisa wa Mahakama huku wanachama na viongozi wa Chadema wakiwa ni wachache tofauti na hapo awali.
Tundu Lissu anakabiliwa na shtaka moja la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, linalotokana na maneno aliyoyatamka kuhusiana na kuzuia kufanyika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.