#HABARI: Mgombea Urais kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Kyara, amesema endapo atapewa ridhaa ya kuingia madarakani ataboresha Sekta ya Mifugo kwa kuimarisha machinjio ya kisasa yatakayosaidia wafugaji kuchinja mifugo yao kitaalamu na kuuza nyama yenye ubora ndani na nje ya nchi. Ameyasema hayo wakati akinadi sera za chama hicho na kuomba kura kwa wananchi ambapo amesema badala ya kuuza ng’ombe wengine watachinja na kuuza nyama jambo ambalo pia litapunguza changamoto ya ajira kwa hapa nchini. Aidha pia ameahidi kumaliza changamoto ya muingiliano wa matumizi ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *