#HABARI: Zaidi ya wanachama 364 wa Chama cha ACT Wazalendo wamehamia rasmi Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakisema wamevutiwa na sera na dira ya Maendeleo inayotekelezwa na CCM chini ya uongozi wa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho.

Wanachama hao wamepokelewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika hafla maalum iliyoambatana na kukabidhiwa kadi mpya za chama, ikiwa ni ishara ya kuanza ukurasa mpya wa kisiasa ndani ya CCM.

Akizungumza mara baada ya kujiunga na CCM, mmoja wa waliokuwa wanachama wa ACT Wazalendo, Naima Ali, alisema uamuzi wake unatokana na kutambua kuwa CCM ina sera thabiti za maendeleo na siyo chama cha chuki.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *