Jeshi la Polisi nchini limesema litawasaka, kuwakamata na kuwafikisha katika mamlaka za haki jinai wote wanaotumia mitandao ya kijamii kuandika, kutengeneza au kusambaza maandishi na picha zenye kuchochea vitendo vya kihalifu.

Msemaji wa Jeshi hilo, DCP David Misime, amesema vitendo hivyo ni kinyume cha sheria na maadili ya Mtanzania, na vimekuwa vikisababisha hofu kwa wananchi wema.

Polisi imesisitiza kuwa operesheni inaendelea na imeonya kuwa hakuna atakayesalimika, kwani watuhumiwa wote watafikishwa kwenye vyombo vya sheria mara ushahidi utakapokamilika.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *