Licha ya kuwepo kwa alama za barabarani zinazowataka madereva kuvuka Daraja la JPM lililopo juu ya Ziwa Victoria kwa mwendo usiozidi kilomita 50 kwa saa, wakazi wa Busisi na watumiaji wa daraja hilo wameelezea malalamiko yao dhidi ya baadhi ya madereva wanaokiuka sheria hizo kwa kuendesha kwa kasi kubwa. Wamesema tabia hiyo inahatarisha usalama wa daraja pamoja na maisha ya watumiaji wengine wa barabara.
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates