Vyombo vya usalama nchini Madagascar, vimewatuhumu waandamanaji kwa kusababisha vurugu wakati wa maandamano ya tangu juma lililopita, vikisema matumizi ya nguvu walizotumia zilisababishwa na tabia zao.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Taifa hilo lililoko kwenye pwani ya bahari ya Hindi, limeshuhudia karibu kila siku ya maandamano ya vijana waliojitokeza barabarani kupinga uhaba wa maji na mgao wa umeme kwenye kisiwa hicho.
Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na polisi na jeshi, wamedai kuwa baadhi ya waandamanaji walijihusisha na vitendo vya kihalifu na hawakuwa tayari kuheshimu maagizo waliyopewa kutawanyika.

Aidha Umoja wa Mataifa umesema watu 22 waliuawa na wengine mamia wakijeruhiwa katika maandamano yaliyoanza Septemba 25, UN ikikosoa matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji.
Taarifa hii imetolewa wakati rais Andy Rajoelina, akifanya mazungumzo na waandaaji wa maandamano hayo kujaribu kutafuta suluhu licha ya shinikizo la kutakiwa kujiuzulu.

Wikendi hii wafuasi wa rais Rajoelina waliandamana kumuunga mkono ingawa hayakuvutia idadi kubwa ya waandamanaji.
Hali ya rushwa nchini humo imeenea kwa kiwango kikubwa, taifa hilo likiorodheshwa katika nafasi ya 170 kati ya mataifa 180 yaliyokithiri kwa rushwa duniani, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Transparency International.