Mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, amesema amekwenda jijini Mwanza kwa ajili ya kusaidia kusaka kura za ushindi kwa mgombea urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.
Akizungumza na viongozi wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Makonda amewataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi katika kampeni.
Dkt. Samia anatarajiwa kuanza rasmi kampeni zake za Kanda ya Ziwa jijini Mwanza kesho Kesho Oktoba 7, 2025.
✍ Mwandishi Wetu
#AzamTVUpdates