Mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu amesema endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atasitisha kila aina ya bugudha na utitiri wa tozo unaoyakabili makundi yasiyo rasmi yanayojihusisha na shughuli halali za kujipatia kipato.

Amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha mazingira bora ya biashara ndogo ndogo na kukuza uchumi wa wananchi wa kipato cha chini.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *