Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Makini, Costar Kibonde, amesema kipaumbele cha chama chake ni kuanzisha viwanda vya kisasa vya uvuvi na kilimo, hatua inayolenga kuongeza tija na kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi.

Kibonde ameeleza kwamba sera hiyo itasaidia kuongeza ajira, kuboresha uchumi wa familia, na kuhakikisha rasilimali za wanyama na mimea zinatumika kwa ufanisi zaidi.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *