Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Chirukile, amewashauri mafundi ujenzi mkoani Rukwa kuungana kwa pamoja ili kupata elimu zaidi inayoendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kupitia vyuo vya VETA na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST), ambavyo vitawajengea maarifa mapya badala ya kuendelea kufanya kazi kwa mazoea.

Akifungua mafunzo kwa mafundi hao yaliyoandaliwa na taasisi ya Magic Builders Foundation, Mkuu huyo wa Wilaya amesema mafundi wengi wamekuwa wakikosa fursa za kupata miradi mikubwa ya ujenzi ya serikali kutokana na kuwa na ujuzi mdogo, hali inayosababisha baadhi yao kufanya kazi chini ya kiwango.

Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *