Nchi ya Rwanda, imeukosoa utawala wa Kinshasa kwa kuendelea kukwamisha utekelezwaji wa baadhi ya vipengele muhimu vya mkataba waliotiliana saini hivi karibuni, utawala wa Kigali ukitoa sababu za kwanini pande hizo hazikutiliana saini makubaliano rasmi katika mazungumzo yaliyopita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe alipongeza ujumbe wa nchi yake ambao ulishiriki katika mazungumzo ya kupata makubaliano ya mfumo wa kiuchumi wa kikanda licha ya kwamba mpango wenyewe haukutiwa saini.

Mpango huu ambao ni sehemu ya mazungumzo yanayoratibiwa na Marekani kujaribu kuzipatanisha pande hizo ulishuhudia utawala wa Kigali na Kinshasa wakikubaliana kimsingi kushauriana kwenye maeneo kadhaa ya kiuchumi.

Watu walio karibu na utawala wa Kinshasa wanasema nchi hiyo haikutia saini makubaliano hayo kwa madai kuwa Rwanda haijaacha kuwasaidia waasi wa M23 wala kuanza kuondoa wanajeshi wake mashariki mwa DRC.

Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa utiaji saini wa makubaliano kati ya Rwanda na DRC.
Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa utiaji saini wa makubaliano kati ya Rwanda na DRC. © Manuel Balce Ceneta / AP

Hata hivyo madai ya DRC, yametupiliwa mbali na waziri wa mambo ya kigeni wa Rwanda Olivier Nduhungirehe, aliyedai ni Kinshasa inayokwamisha, akitolea mfano kilichotokea Luanda, ambapo licha ya ujumbe wa Kinshasa kukubali serikali kuwanyanganya silaha waasi wa FDLR, rais Tschisekedi akaagiza wasitie saini.

Kutotiwa saini kwa makubaliano haya kunauweka mpango wa Marekani inayolenga kunufaika na madini kutoka mashariki mwa Congo kwenye sintofahamu, kila upande ukimtuhumu mwingine kukwamisha makubaliano rasmi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *