
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House, Trump alisema, kwake linaonekana kama wazo zuri, alipoulizwa kuhusu pendekezo hilo, miezi minne kabla ya mkataba huo wa New START kufikia ukomo Februari 6 mwaka 2026. Mkataba wa New START, uliotiwa saini mwaka 2010, unalenga kupunguza idadi ya silaha za nyuklia za kushambulia kwa pande zote mbili. Unaruhusu kila nchi kuwa na vichwa vya nyuklia 1,550 vilivyotumika, pamoja na makombora na mabomu mazito 800. Pia unatoa fursa ya ukaguzi wa pamoja ili kuhakikisha utekelezaji wake.Hata hivyo, ukaguzi huo umesitishwa tangu Urusi ilipojiondoa kwenye mkataba huo miaka miwili iliyopita, kufuatia vita vya Ukraine na mvutano unaoongezeka kati ya Moscow na mataifa ya Magharibi.