Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ametangaza Baraza jipya la Mawaziri, litakaloongozwa na Waziri Mkuu Sébastien Lecornu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja, wakati huu serikali ya rais Macron ikikabiliwa na changamoto kubwa ya kisiasa, baada ya wabunge kukataa kupitisha mpango wake wa kubana matumizi, na kuzua maandamano makubwa ya mara kwa mara nchini humo.

Waziri mpya wa Uchumi ni Roland Lescure, anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuja na bajeti ya mwaka ujao, itakayokubaliwa na bunge.

Naye, Waziri wa zamani wa Uchumi, Bruno Le Maire, aliyeshika nafasi hiyo kati ya mwaka 2017  hadi 2024, ameteuliwa kuwa Waziri mpya wa Ulinzi.

Hata hivyo, Bruno Retailleau amebaki kama Waziri wa Mambo ya ndani, sawa na Jean-Noël Barrot, anayesalia katika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya nje.

Jordan Bardella, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha National Rally, amesema mabadiliko haliyofanywa hayaonekani kuleta matumaini na kutishia kuwa serikali hii mpya huenda ikakabiliwa na kura ya kukosa imani hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *