Wachimbaji wadogo zaidi ya 500 wa kijiji cha Mwaoga, wilayani Chunya wameandamana na kufunga barabara inayoelekea makao makuu ya Kampuni ya Shanta Mine, wakidai kurejeshewa eneo walilokuwa wakichimba dhahabu linalodaiwa kuchukuliwa bila kuwashirikisha.
Mwekezaji huyo anadaiwa kuchukua eneo hilo kwa nguvu, ambalo pia lina makaburi na kuwataka wachimbaji hao kuondoka bila kuelezwa mahali pa kwenda…licha ya malalamiko yao kuwasilishwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi