Wakulima wadogo wa zao la mkonge wilayani Korogwe, mkoani Tanga, wanatarajia kuondokana na changamoto ya mazao yao kuozea shambani baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza wakabidhiwe mashine za kuchakata mkonge zilizokuwa zikiendeshwa na kampuni ya Sisalana.
Wakizungumza na waandishi wa habari, baadhi ya wakulima wamesema changamoto ya mkonge kuozea shambani imekuwa ikiwakwamisha kwa muda mrefu na kupunguza kipato chao.
Wameeleza kuwa hatua ya Serikali ni faraja kubwa itakayoongeza thamani ya mazao yao na kuimarisha uchumi wa kaya.
✍ Mariam Shedafa
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates