#HABARI: Jeshi la Polisi limeanza rasmi uchunguzi wa tuhuma za kutekwa kwa Humphrey Polepole kufuatia madai yaliyotolewa na Augustino Polepole kupitia mitandao ya kijamii, ambapo alidai kuwa ndugu yake alitekwa na Afisa wa Polisi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi hilo iliyotolewa Oktoba 6, 2025, jalada la uchunguzi lilifunguliwa mara moja siku hiyo hiyo, na hatua za awali zimejumuisha ukusanyaji wa taarifa mbalimbali zinazohusiana na tukio hilo.

Polisi wamesema wanaendelea kumtafuta Augustino Polepole ili aweze kutoa ushirikiano na kufafanua kwa kina madai yake, ikiwa ni pamoja na kutoa uthibitisho kuwa Humphrey alikuwa mkazi au mpangaji wa nyumba aliyodai kuwa tukio hilo lilifanyika.

Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi huu ukiendelea na limeahidi kutoa taarifa zaidi kadri hatua za kisheria zitakavyopigwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *