#HABARI: Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu, amewataka viongozi wanawake chipukizi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika kuchukua hatua madhubuti na kuleta mabadiliko halisi katika safari zao za uongozi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tano wa uongozi wa wanawake ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute), Dkt. Jingu amesisitiza umuhimu wa kutumia maarifa waliyonayo kuleta ushawishi na matokeo chanya katika jamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Uongozi Institute, Kadari Singo, amesema taasisi hiyo imezindua mpango maalum wa wanawake katika uongozi, ambao umelenga kuongeza uwakilishi wa wanawake katika nafasi za juu za kisiasa, kiuchumi na kibiashara na kuongeza kuwa takwimu za Kimataifa zinaonesha ni asilimia 33 tu ya wanawake wanaoshikilia nafasi kubwa za maamuzi duniani.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania