#HABARI: Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe imemhukumu Athumani Bakari Mbagando kifungo cha miaka 20 Jela baada ya kutiwa hatiani kwa kukutwa na miguu minne ya Twiga, vipande 2 vya ngozi ya Twiga vyote vikiwa na thamani ya fedha za Tanzania Milioni hamsini na nne, laki sita, hamsini na moja elfu na mia nane.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe Nsangalufu ameeleza kuridhishwa na ushahidi wa upande wa Jamhuri na kwamba hukumu hiyo ameitoa ili iwe fundisho kwa wananchi wengine wenye tabia ya kuingia kwenye maeneo ya hifadhi na kutenda makosa kama aliyotenda mtuhumiwa huyo.

Awali mtuhumiwa aliiomba Mahakama hiyo kumuonea huruma na kumpunguzia adhabu kwa kuwa ana familia inayomtegemea na ni kosa lake la kwanza.

Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 05 Oktoba 2024 huko katika eneo Hifadhi ya Mwalimu Nyerere, Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *