#HABARI: Mkurugenzi wa Nishati safi ya Kupikia, Nolasco Mlay pamoja na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati wameanza ziara ya kikaz…#HABARI: Mkurugenzi wa Nishati safi ya Kupikia, Nolasco Mlay pamoja na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati wameanza ziara ya kikaz…

#HABARI: Mkurugenzi wa Nishati safi ya Kupikia, Nolasco Mlay pamoja na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati wameanza ziara ya kikazi mkoani Mwanza kwa lengo la kukagua utekelezaji wa agizo la Serikali kwa Taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 kutumia Nishati Safi ya Kupikia.

Ziara hiyo imeanza kwa kukagua shule tatu za Sekondari katika Manispaa ya Ilemela ambazo zimeanza kutumia Nishati Safi ya Kupikia baada ya kunufaika na mradi wa CookFund kupitia mpango wa kimataifa wa Integrated Approach to Sustainable Clean Cooking Solution unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU).

Ziara hiyo pia inalenga kufanya tathmini ya matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa taasisi zinazopokea ufadhili kutoka mradi wa CookFund.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bw. Nolasco Mlay amesema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024–2034), ambao unalenga kuhakikisha taasisi za umma ikiwemo shule, zinatumia teknolojia salama na rafiki kwa mazingira katika upishi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *