#HABARI: Mwakilishi wa Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Tanzania, Bw. Abdillahi Mutabazi, amevitaka vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) kutokata tamaa katika utendaji kazi wao wa kila siku huku akimtolea mfano wa kuigwa Mwandishi wa Habari wa ITV/RADIO ONE mkoa wa Lindi, Bi. Fatuma Maumba ambaye hivi karibuni Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) ilimpatia tuzo ya Mwanahabari Bora wa Taarifa za Korosho katoka kundi la Televisheni Msimu wa Mwaka 2024/2025 aliyokabidhiwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe jijini Dodoma Agosti 22, 2025.
Mwakilishi wa Mrajis ameyasema hayo mkoani Lindi wakati akizungumza na mameneja pamoja na wahasibu kutoka vyama vya msingi vya ushirika vya Halmashauri ya Mtama, Kilwa na Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ambao wamehitimu mafunzo yao ya program maalum ya utunzaji wa uandishi wa vitabu vya hesabu za vyama vya msingi vya ushirika (PUVU).
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.