Mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuendelea kulinda na kuheshimisha jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani na nje ya nchi endapo ataaminiwa kuongoza kwa muhula mwingine.

Akizungumza leo Jumanne, Oktoba 7, 2025, mbele ya maelfu ya wananchi wa wilaya za Buchosa na Sengerema mkoani Mwanza, Dkt. Samia amesema heshima ya Tanzania itaendelea kudumishwa kwa kuimarisha misingi ya haki, kufanya chaguzi huru na za amani, kufuata sheria, na kuendeleza diplomasia yenye tija kimataifa.

Alisisitiza kuwa serikali yake itahakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya, maji safi na salama, elimu bila ubaguzi, na kuendeleza sekta zote zinazochochea uchumi wa taifa.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *