Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi nchini (TISEZA), Gilead Teri amesema zaidi ya shilingi trilioni sita zimepatikana kati ya mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu kupitia miradi 201 iliyowekezwa katika mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha ripoti ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/26 kuhusu hali ya uwekezaji nchini, Teri alisema zaidi ya ajira 200 zimezalishwa kutokana na uwekezaji huo.

Ameongeza kuwa katika kipindi hicho, idadi ya miradi inayomilikiwa na wawekezaji wa kigeni imeongezeka kutoka miradi 70 (sawa na asilimia 27) hadi miradi 74 (sawa na asilimia 35), ikionesha ongezeko la uwekezaji wa kimataifa nchini.

#AzamTVUpdates
✍Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *