#HABARI: Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, TANESCO imekuja na program maalumu ya kuwahudumia wateja wao kwa kuwaunganishia wateja wapya huduma ya umeme ndani ya siku moja, ikiwa ni sehemu ya kusogeza huduma karibu na wateja wao.

Akizungumza katika maadhimisho hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam Bi. Gowelle ameeleza kuwa TANESCO imekuja na program hiyo ya TANESCO Mtaani kwako kwa lengo la kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wafanyakazi muhimu wa vitengo mbalimbali vya shirika wameweka kambi kwenye viwaja hivyo kwa siku tatu kuanzia leo Oktoba 08 ili kutoa huduma kwa wananchi.

‘’TANESCO tumeona tuadhimishe wiki ya huduma kwa mteja kwa kusogeza huduma kwa jamii, tumekuja na program ya TANESCO Mtaani kwako kwa lengo la kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam, ni fursa ya pekee kwa wananchi kufika katika viwanja hivi vya Mwembe Yanga kupata elimu na mambo mbalimbali yahusuyo Shirika,’’alisisitiza Bi Gowelle.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *