#HABARI: Mahakama ya Hakimu MKazi Bukoba Mfawidhi Mh. Massesa – PRM katika shauri la Rushwa namba 24339/2025 imemtia hatiani aliyekuwa Mlinzi Mkuu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera Bw. Warioba Nzwili Sayi kwa makosa ya Rushwa.

Chini ya kifungu cha 15 PCCA Mshtakiwa huyo kwa njia ya rushwa alijipatia kiasi cha 4,000,000 kutoka kwa Emiliana Jema Shibumbila ili aweze kumpatia mtoto wake ajira. Hii ni baada ya kujifanya kwamba yeye ni Afisa Utumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Baada ya Mshtakiwa kutiwa hatiani ametakiwa kulipa fine ya Tsh. 500,000 au kwenda Jela mwaka mmoja na kutakiwa kurejesha kiasi cha Tsh. 4,000,000 alichojipatia kwa njia ya rushwa kwa mlalamikaji Bi. Emiliana Shibumbila ndani ya miezi mitano.

Mshtakiwa amelipa faini.
Shauri hili liliendeshwa na waendesha mashtaka wa TAKUKURU Wakili William Fussi na Daudi Jacob Oringa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *