#HABARI: Mbunge wa Viti Maalum Mstaafu, Felista Njau, amewataka wabebaji mizigo wa Mji Mdogo wa Mbulu kuungana kumuunga mkono Mgombea wa nafasi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu ujao, akisema kuwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta za afya, biashara na utalii ni ushahidi wa uongozi wenye dira, huruma na utu.
Akizungumza na wabebaji wa mizigo katika kituo cha mabasi cha Mbulu, Njau alisema Serikali ya awamu ya sita imejipambanua kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi wa kipato cha chini, ikiwemo ujenzi wa vituo vya afya, maboresho ya zahanati na nyumba za wazazi, hatua zilizosaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto nchini.
“Mama huyu ni kiongozi mwenye huruma na maono. Amefanya makubwa ndani ya miaka minne na nusu – tusiache kupiga kura tukiwa mashuhuda wa maendeleo haya,” alisema Njau.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.