#HABARI: Serikali imeeleza mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji ambapo Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imefanikiwa kufikisha huduma ya umeme kwenye vijiji vyote 12,318 sawa na asilimia 100 na miradi ya umeme kwenye vitongoji inatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2030.
Mafanikio ya miradi ya umeme Vijijini yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Umeme Vijijini Mha. Jones Olotu wakati akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja jijini Dodoma.
“Tanzania bara tuna jumla ya vitongoji 64,359 ambapo kati ya hivyo vitongoji 37,328 sawa na asilimia 58 vimeshafikiwa na huduma ya umeme na bado miradi ya kusambaza na kufikisha huduma ya umeme inaendelea katika maeneo mbalimbali nchini,” amesema Mha. Olotu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.