
Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Manchester United Josua Zirkzee ,24,anatafuta upenyo wa kuondoka mwezi Januari kama njia muhimu ya kujumuishwa katika kikosi cha taifa cha Uholanzi kwenye kombe la dunia mwakani. (Mail Plus)
West Ham wana azma ya kumsajili Zirkzee huku meneja Nuno Espirito Santo akipanga kuinoa safu yake ya mashambulizi. (Football Insider)
Mkufunzi wa England Kobbie Mainoo,20, nae pia anataka kuondoka Manchester United na kuelekea Napoli lakini itabidi asubiri hadi Januari.
Harry Maguire ,32, ana hamu ya kuendelea kusalia Manchester United lakini itamgharimu kwani atalazimika kupunguziwa mshahara iwapo atasalia hapo hadi mwisho wa msimu. (Talksport)
Meneja wa Chelsea Enzo Maresca hana mpango wa kumrejesha kikosini mlinzi wa Ufaransa Axel Disasi ,27, licha ya majanga ya majeruhi aliyonayo kwa sasa. (SUN)
Leeds United iko shughulini kumtafuta winga mwezi Januari baada ya kufeli kumsajili Harry Wilson wa Fulham ,28, siku ya mwisho ya uhamisho(Sky sports)
Wing awa zamani wa Leeds United Raphinha yupo kwenye darubini la Manchester United baada ya kutesa sana akiwa Barcelona lakini mbrazili huyo,28,huenda akawagharimu pauni milioni 120. (Fichajes)

Chanzo cha picha, Getty Images
Aliyekuwa meneja wa Everton Sean Dyce hana azma yoyote ya kuchukuwa kibarua cha Rangers ya Uskwochi baada ya kupigwa kalamu kw akocha Russell Martin. (Sky sports)
Imetafsiriwa na Ahmed Bahajj na kuhaririwa na Ambia Hirsi