
Chanzo cha picha, Getty Images
Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance anasema Rais wa Marekani Donald Trump anafikiria kuipa Ukraine makombora ya masafa marefu aina ya Tomahawk.
Ukraine imekuwa ikiwaomba washirika wake wa Magharibi kuipatia silaha zenye uwezo wa kushambulia miji ya Urusi kwa umbali mrefu.
Ukraine inaamini kwamba kupatikana kwa silaha hizo kungedhoofisha sana tasnia ya kijeshi ya Urusi na kumaliza vita.
“Ikiwa gharama ya kuendeleza vita itaongezeka kwa Moscow, italazimika kuanza mazungumzo ya amani,” Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Ivan Havrilyuk aliambia BBC.
Msemaji wa Kremlin Dmitry Pekov hata hivyo alipuuzilia mbali matamshi ya Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance akisema: “Kiev haina muafaka.
“Tomahawks au aina nyingine za makombora, haziwezi kubadilisha mwenendo wa vita ,” aliongeza.
Mjumbe Maalum wa Marekani kwa Ukraine, Keiz Kelong anasema kwamba Trump ndiye aliamuru shambulio hilo ndani kabisa ya mipaka ya Urusi.
Maoni ya Vance na Kelong yanawiana na mabadiliko ya hivi majuzi katika msimamo wa utawala wa Marekani kuhusu vita hivyo.
Makombora ya Tomahawk ni nini, na yanafanyaje kazi?
Makombora ya Tomahawk ni dhaifu ukilinganisha na makombora ya hali ya juu na masafa marefu , na hutumiwa hasa na Marekani na Uingereza kushambulia pasi na kukosea shabaha.
Hufyatuliwa kutoka kwenye meli au chombo cha chini ya maji, makombora hayo hulenga juu umbali wa wastani ili kuepuka kudunguliwa na adui.
Njia ya makombora inaweza kuhuishwa kwa wakati halisi kupitia viungo vya data, na inapohitajika, inaweza kurejelewa au (kurekebishwa) na kutumwa kwa madhumuni tofauti.
Makombora ya Tomahawk pia yanaweza kufyatuliwa kutoka kwenye meli , chini ya maji au kufyatuliwa kwa mfumo wa wima.
Hivyo, inapokuwa katika njia yake , inafikia eneo lengwa kwa kasi ya takriban 880 km/h kwa saa.
Makombora husafiri kwa mwinuko mdogo (takriban mita 30–50 juu ya ardhi) na huruka kwa mwendo wa polepole badala ya moja kwa moja, jambo linalofanya iwe vigumu kwa rada kugundua na kuzikamata.
Kwa nini Ukraine inahitaji makombora haya?
Kombora hilo huruka kwa masafa marefu, kwa kawaida hufyatuliwa kutoka baharini na kulenga shabaha iliyokusudiwa mbali zaidi ya uwanja wa vita.
Silaha hiyo inaweza kugonga kwa wastani wa kilomita 1,600 hadi 2,500.
Kipengele kingine cha kutofautisha ni kwamba inashambulia kwa usahihi hata ndani ya kile kinachoaminika kuwa anga yenye ulinzi imara.
Ukraine inaiomba Marekani ikiamini kuwa itaweza kushambulia miji ya Urusi kutokea mbali.
Kombora ambalo Ukraine inatarajia litakuwa na urefu wa mita 6.1.
Tomahawk,aina hiyo ya kombora pia ina uzito wa kilo 1,510.
Kwa mujibu wa data ya Pentagon, Marekani inapanga kununua makombora 57 hadi kufikia mwisho wa mwaka huu kwa wastani wa gharama ya $1.3 milioni kwa kipande.
Wakati jitihada zikifanyika mamilioni ya dola yametengwa kuboresha na kuimarisha silaha, ikijumuisha mifumo ya uongozaji.
Jeshi la Marekani na washirika wake wamefanya utafiti na kuboresha GPS kusaidia makombora ya Tomahawk na kutumia wakati jeshi la wanamaji wa Marekani na Uingereza walipofyatua makombora ya Tomahawk dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen.
Swala ibuka ni kwa namna gani Tomahawk itatofautiana na makombora ya sasa ya Ukraine?
Ukraine kwa sasa ina idadi kubwa ya makombora ya kurusha kwa masafa marefu yaliyotengenezwa na kutolewa na nchi za Magharibi.
Flamingo -Fire Point ya Ukraine hivi karibuni ilizindua kombora la Flamingo, ambalo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alilielezea kuwa silaha yenye mafanikio inayozalishwa nchini humo.
Ikiwa na safu ya zaidi ya maili 1,000, Ukraine iliripoti matumizi yake ya kwanza mnamo Agosti 2025.
Neptune -kutoka Ukraine ilitengeneza na kuzindua kombora la kupambana na meli mnamo 2015.
Makombora ya kwanza na yaliyofuata ya aina hii yalikuwa na takriban maili 600.
Harpoon – Imetengenezwa Marekani na Boeing, Harpoon ni kombora la hali ya juu , la kuzuia meli ambalo hutumia rada kuruka juu kidogo ya maji ili kukwepa vizuizi vya kiulinzi.
Inaweza kufyatuliwa kutoka kwenye meli, manowari, ndege au pwani na kusafiri umbali wa maili 75 usawa wa bahari.
ATACMS – Iliyoundwa na Lockheed Martin Corp (LMT.N), Mfumo wa makombora yanayotumika kijeshi yenye upeo wa juu wa hadi maili 190 kwa mujibu wa muundo wake.
Ni kombora la mfumo wa kuanzia chini hadi ardhini lenye kwenda masafa ya wastani, na urefu wa takriban mita 4.
ATACMS inaweza kufyatuliwa kutoka kwenye Mfumo wa roketi wa M270 (MLRS) au Mfumo wa Roketi wa Kisasa wa M142 (HIMARS).
Makombora ya Dhoruba – yaliyotengenezwa na MBDA ya Ulaya, makombora kama hayo yana safu ya maili 155 na uzito wa pauni 990 sawa na silaha za kawaida za kijeshi.