Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana, amesema maboresho yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kujenga mahusiano bora ya kidiplomasia yamechochea ukuaji wa sekta ya utalii Tanzania na kuongeza pato la taifa kupitia watalii wanaoingia nchini.

Dkt. Chana amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum kwa wanafunzi na watendaji wa Chuo cha Taifa cha Utalii, yaliyolenga matumizi sahihi ya teknolojia ya rasilimali zinazotumika katika mahoteli pamoja na utoaji wa huduma za kitalii, ili kuendana na mabadiliko haya na kuvutia watalii zaidi nchini.

#AzamTVUpdates
✍Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *