Zaidi ya wakulima 62,000 wadogo wadogo nchini wamenufaika na mafunzo ya kilimo cha mbogamboga na matunda yaliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti na Uendelezaji wa Kilimo cha Mbogamboga – Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (World Vegetable Center – WorldVeg), ili kuwasaidia kuongeza uzalishaji na kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na wandishi wa habari wakati wa hafla ya kufunga rasmi utekelezaji wa mradi huo, unaoitwa Accelerated Innovation Delivery Initiative (AID-I), Meneja wa Programu Tanzania wa WorldVeg, Colleta Ndunguru amesema mradi huo umekuwa na tija tangu kuanzishwa kwake mwaka 2023 katika mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, pamoja na visiwani Zanzibar.

✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *