Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka wananchi kuwapuuza wanasiasa wasiohubiri amani, akisisitiza kuwa amani ndiyo nguzo kuu ya maendeleo ya taifa.

Akizungumza Oktoba 7, 2025, katika Uwanja wa Michezo wa Likoni, Kojani, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dkt. Mwinyi amesema viongozi wasioweka mbele amani hawana nia njema na ustawi wa nchi.

Akijibu ombi la wananchi wa Kojani, Dkt. Mwinyi ameahidi kujenga uwanja wa michezo kisiwani humo ili kukuza vipaji vya vijana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *