
Erdogan apongeza makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza, na kusifu nafasi ya Misri na Qatar
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameeleza kufurahishwa na makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na Israel huko Gaza kufuatia mazungumzo yaliyoandaliwa Sharm el-Sheikh akisisitiza kuwa nchi yake imechangia katika kufanikisha hilo.