Mapema mwezi huu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia ilituma barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ikiishutumu Eritrea kwa kushirikiana na Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray, TPLF kwa kutaka ”kuanzisha vita”.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia, Eritrea na TPLF zimekuwa zikiyafadhili, kuyahamasisha na kuyaelekeza makundi yenye silaha katika jimbo la Amhara, ambako jeshi la Ethiopia limekuwa likikabiliana na waasi kwa miaka kadhaa.

Madai yasiyo na ukweli

Waziri wa Habari wa Eritrea, Yemane Ghebremeskel amesema Alhamisi kuwa barua hiyo ni ya ”udanganyifu”.

Yemane ameishutumu Ethiopia kwa kupanga njama za kuudhofisha ”uhuru wake uliopatikana kwa juhudi kubwa” kwa kujaribu kujipatia nafasi ya kuifikia bandari yake.

Katika miaka ya hivi karibuni mvutano umekuwa ukiongezeka kati ya mataifa hayo mawili jirani ya Pembe ya Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *