#HABARI:Ikiwa leo ni siku ya nne ya usikilizwaji wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Tundu Lissu, katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ndogo ya Dar es Saalam, imeanza ambapo kabla ya kesi hiyo kuanza kutolewa ushahidi Mh Lissu alilalamikia kitendo cha kuendelea kuzuiwa kwa badhi ya watu kuingia katika ukumbi wa mahakama kusikiliza kesi

Akasema kuwa inaonyesha maagizo yanayotolewa na mahakama kuwa watu waruhusiwe hayafanyiwa kazi na inaonekana wapo watu wengine ambao wananguvu kuliko mahakama hatua ambayo inashushuha hadhi ya mahakama hiyo.

Aidha Mh Lissu akaongeza kuwa hataacha kulizungumzia jambo hili kwani halipo sawa kisheria.

Kufuatia hoja hiyo ya Mh Lissu kupitia Mh Jaji Dunstan Ndunguru kiongozi wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo akasema kesi iendelee jambo hilo atalitolea ufafanuzi baadaye.

Kesi tayari leo imeanza ambapo shahidi wa kwanza amekuja kuulizwa maswali ya ufafanuzi kwa upande wa Jamhuri,shahidi huyo anaitwa George Bagyemu ambaye ni Naibu Mkuu wa Upepelezi Kanda Maaluum ya Dar es Salaam na ambaye ni Kamishna Msaidizi wa Polisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *