#HABARI:Mama yake Humprey Polepole tayari amewasili katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam Katika shauri la kutekwa kwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, limeitwa Mahakamani Kuu Masjala ndogo ya Dar es salaam ambapo muda wowote kuanzia sasa usikilizwaji kwa hatua ya awali uanatarajia kufanyika.

‎Shauri hilo la maombi ya amri ya kufikishwa mahakamani kwa lugha ya kisheria ‘Habeas Corpus’ limefunguliwa na Mawakili wa Polepole, wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala kwa niaba yake Polepole.

‎Katika shauri hilo wajibu maombi ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum Dar es Salaam (ZCO) na Kamanda wa Polis Kanda Maalum Dar es Salaam (ZPC).

‎Shahauri hilo limepangwa kusikilizwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam, Salma Maghimbi.

‎Kwa mujibu wa wito huo shauri hilo limeitwa mbele ya Jaji Maghimbi leo Alhamisi, Oktoba 9, 2025

‎Shauri hilo lilifunguliwa mahakamani hapo Oktoba 7 , 2025, chini ya hati ya dharura.

‎Katika hati hiyo ya dharura Wakili Kibatala anaeleza kuwa tangu Oktoba 6, 2025, Polepole aliripotiwa kutekwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni maofisa wa Jeshi la Polisi waliovamia nyumbani kwake Ununio, Wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

‎Pia wakili Kibatala anadai kuwa mpaka sasa hajashtakiwa kwa kosa lolote la jinai, katika mahakama yoyote ya kisheria na kwamba inaaminika kuwa amewekwa kizuizini mahali kusikojulikana na wajibu maombi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *