
Chanzo cha picha, Getty Images
Siku moja mnamo mwaka 2005, hospitali ambayo daktari wa magonjwa ya akili David Avery alifanya kazi huko Seattle, USA, alimlaza mgonjwa wa miaka 35 ambaye alikuwa mhandisi na alipenda kuangazia hisabati.
Mgonjwa aliteseka kutokana na mabadiliko ya mhemko kutoka hatua moja hadi nyingine ikiwa ni pamoja na kuona na kusikia vitu ambavyo havikuwepo, kuwa na mawazo ya kujiua, na kuwa na shida ya kupata usingizi, kuanzia kukosa usingizi hadi kulala masaa 12 kwa siku.
Akiwa msuluhishi mwenye bidii wa hesabu, mgonjwa huyu aliweka rekodi kwa uangalifu za dalili zake katika jitihada za kuelewa asili ya magonjwa yake. Avery alifuatilia kwa karibu rekodi hizi na akasema alishangazwa sana na mara ambazo mabadiliko hayo yalitokea.
Mabadiliko katika usingizi na hisia yalionekana kwendana na mabadiliko ya kuandama kwa Mwezi au kutoka Mwezi mpevu hadi Mwezi kamili.
Mwanzoni, Avery alikataa kuamini uchunguzi huu. Hata kama mhemko wa mgonjwa unabadilika kwendana na mwezi, hakuwa na njia ya kuelezea kwa nini iwe hivi, wala wazo lolote la jinsi ya kukabiliana na hali hiyo.
Mgonjwa alitibiwa kwa mwanga na madawa, na daktari wake aliweka maelezo ya mgonjwa katika droo na kuyafungia.
Miaka 12 baadaye, daktari mashuhuri wa magonjwa ya akili aitwaye Thomas Wehr alichapisha utafiti wa watu 17 wenye matatizo ya kisaikolojia, ambapo hisia za wagonjwa hubadilika kati ya unyogovu na kuwa kama mwenye matatizo ya akili haraka zaidi kuliko kawaida.
Wagonjwa kama Avery, walionyesha hali isiyo ya kawaida katika muda wanakuwa wanapougua.
Kilichomvutia zaidi kuhusu hili, Weir alisema, ilikuwa usahihi wa hali ya juu wa jinsi hali yake ilivyokuwa ikitokea kulingana na Mwezi ulivyo, kwa njia ambayo mtu hangetarajia kutoka kwa mchakato wa kibaolojia.
Hii ilimfanya ajiulize kama kulikuwa na ushawishi wa nje unaodhibiti hali zao za kiafya.
Alizungumzia suala hili, athari za Mwezi zilimjia akilini mwake kutokana na imani iliyokithiri katika baadhi ya zama kwamba Mwezi unaathiri tabia ya mwanadamu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa karne nyingi, watu wameamini kwamba Mwezi huathiri tabia ya mwanadamu. Mwanafalsafa wa Kigiriki Aristotle aliamini kwamba Mwezi unaathiri hali ya “wazimu” na kifafa. Wanawake wajawazito pia walidaiwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kuzaa wakati wa Mwezi unapokuwa mzima, ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi wa hili.
Pia hakuna ushahidi wa kuhusisha awamu fulani za Mwezi na ongezeko la jeuri miongoni mwa wafungwa au wale wanaougua ugonjwa wa akili, ingawa uchunguzi wa hivi majuzi unapendekeza kwamba vitendo vya uhalifu wa nje—kwa mfano barabarani au kwenye fuo—vinaweza kuongezeka kunapokuwa na mwangaza wa mwezi.
Hata hivyo, kuna baadhi ya ushahidi wa kisayansi kwamba mifumo ya usingizi hutofautiana kulingana na mzunguko wa Mwezi au awamu ya mwezi.
Utafiti wa 2013 uliofanywa chini ya hali zilizodhibitiwa kabisa, kama vile maabara ya kuchunguza hali za usingizi, ulibaini kuwa watu walichukua dakika tano zaidi kusinzia na kulala kwa takriban dakika 20 kwa siku karibu na Mwezi kuwa mzima kuliko siku zingine za mwezi, hata kama hakukuwa na mwangaza wa mwezi.
Utafiti huo pia umebaini kuwa kiwango cha usingizi mzito waliopata kilipunguzwa kwa asilimia 30. Hata hivyo, uchunguzi uliofuata haukufikia hitimisho sawa na maoni hayo.

Chanzo cha picha, Alamy
Mwezi huathiri dunia kwa njia kadhaa, ya kwanza na ya wazi zaidi ambayo ni kiasi cha mwanga ambacho hutoa, ambacho hubadilika Mwezi mzima. Unakuwa umejaa kila baada ya siku 29.5, na Mwezi mpya unaonekana siku 14.8 baada ya Mwezi kamili.
Kwa kuongezea, kuna mvutano wa mwezi, ambao hutoa mawimbi ya bahari kila baada ya masaa 12.4. Mawimbi haya hufika kilele takriban kila baada ya wiki mbili, wakati mwingine hutokea kila baada ya siku 14.8 kutokana na mvutano wa Mwezi na jua, na nyakati nyingine hutokea kila baada ya siku 13.7 kutokana na nafasi ya Mwezi kuhusiana na ikweta ya Dunia.
Inashangaza, hii ilikuwa sawa sawa na hali ya wagonjwa katika utafiti wa Weir.
Mara tu Avery aliposoma kuhusu utafiti huo, alimpigia simu Weir, na hao wawili baadaye wakachambua upya data kutoka kwa mgonjwa injinia tuliyemtaja hapo awali, na kugundua kwamba mabadiliko ya hisia zake yalilingana na mzunguko wa siku 14.8.
Anne Werz-Justice, mtaalam wa kronobiolojia katika Hospitali ya Akili ya Chuo Kikuu cha Basel nchini Uswizi, anaangazia uhusiano kati ya mizunguko ya Mwezi na mizunguko ya unyogovu na wazimu “ya kuaminika na yenye kuzua utata.” “NI vigumu kujua utaratibu unaoendelea,” anasema.
Kinadharia, mwangaza wa mbalamwezi unaweza kutatiza usingizi wa watu, na hivyo kuathiri hisia zao. Hii ni kweli hasa kwa watu walio na ugonjwa wa kubadilika-badilika hisia, hadi kuna ushahidi wa kisayansi wenye kusema kuwa ukosefu wa usingizi kunaweza kutumiwa kuwatoa watu wa aina hii kutoka kwa unyogovu.
Lakini Weir aliendelea kusadiki kwamba mwanga wa Mwezi haungeweza kuwa na ushawishi mkubwa juu ya tabia ya mwanadamu.
Weir anaamini kwamba mvutano wa Mwezi ndio unaoweza kuathiri tabia na hisia za binadamu.
Lakini bado haijulikani ikiwa ushawishi wa Mwezi katika muktadha huu ni muhimu vya kutosha kusababisha mabadiliko ya kibiolojia kwa wanadamu.
Hata hivyo, baadhi ya tafiti zimehusisha shughuli za jua na viwango vya kuongezeka kwa watu kujiua, magonjwa ya moyo, kiharusi, kifafa, na skizofrenia.
Lakini Robert Weeks, mtaalam katika Chuo Kikuu cha London, anasema tatizo ni kwamba utafiti wa kisayansi juu ya hilo ni kidogo sana kwamba ni vigumu kupata matokeo yoyote ya uhakika.