Mchambuzi wa Kimataifa, Pater Nusniyegira akizungumza mapema leo kwenye kipindi cha #MoriningTrumpet, amesema kushuka kwa uchumi wa kijamii kwa taifa la Ufaransa ndio sababu inayowaondoa madarakani na kujiuzuru kwa mawaziri wake wakuu kabla ya muda kuisha.

Ikumbukwe kuwa tangu Rais Emmanuel Macron aingie madarakani mwaka 2017, Ufaransa imeshuhudia mawaziri wakuu saba, ambao wote walijiuzuru, huku watano kati yao wakiondoka ndani ya miaka mitatu iliyopita.

✍Nifa Omary
Mhariri | @abuuyusuftz

#AzamTVUpdates #MorningTrumpet #utv108

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *