Mwezi Juni, Marekani iliweka vikwazo kwa serikali ya Sudan inayoshirikiana na jeshi kutokana na matumizi ya silaha za kemikali, lakini haikufafanua wapi na lini walizitumia.

Uchunguzi uliofanywa na Shirika la habari la France24, umeonyesha kuwa jeshi linaonekana kudondosha mapipa mawili yenye klorini Septemba 2024 karibu na kiwanda cha mafuta cha Al-Jaili kaskazini mwa Khartoum.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limesema matumizi ya kemikali ya viwandani kama silaha, yanasababisha hali ya wasiwasi.

Sudan imerudia kukanusha madai ya Marekani, ikiyaita ”yasiyo na msingi” na ”kitisho cha kisiasa”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *