Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa ambaye hakutaka kutajwa jina, amesema vikosi hivyo vitapunguzwa kutokana na ukosefu wa fedha, unaohusishwa zaidi na kupunguzwa kwa misaada ya Marekani.

Takribani wanajeshi na askari polisi 13,000 hadi 14,000, pamoja na vifaa vyao watarudishwa makwao, huku idadi kubwa ya wafanyakazi wa kiraia wa vikosi hivyo pia ikiathiriwa.

Marekani kulipa nusu ya dola bilioni 5.4

Marekani ilikuwa inatarajiwa kuchangia dola bilioni 1.3 kati ya jumla ya bajeti ya dola bilioni 5.4 kwa shughuli za kulinda amani za 2025 hadi 2026.

Hata hivyo, Marekani imeueleza Umoja wa Mataifa kwamba italipa tu nusu ya kiasi hicho, au dola milioni 682  ambazo zinajumuisha dola milioni 85 zilizotengwa kwa ajili ya kikosi kipya cha kimataifa cha kupambana na magenge ya uhalifu nchini Haiti, ambacho hakikuwepo katika bajeti ya awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *