Msemaji wa OCHA, ameyasema hayo Alhamisi baada ya Israel na Hamas kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano katika awamu ya kwanza ya mpango wa amani wa Gaza.

Amesema mara tu maafisa wa Israel watakapotoa idhini, misaada hiyo inaweza kupelekwa kwa watu wenye uhitaji.

Amesema misaada hiyo ni pamoja na chakula, dawa, mahema na misaada mingine inayohitajika haraka.

Asilimia 45 ya magari ya misaada imezuiwa

Mapema wiki hii, OCHA ilisema maafisa wa Israel ama hawajaidhinisha au wamezuia asilimia 45 ya magari yake ya misaada yaliyoorodheshwa tangu vita vilipoanza Oktoba, 2023.

Amesema ili kutoa msaada kwa raia, OCHA inahitaji maeneo ya kuvukia ya mipakani yawe wazi, usalama kwa wafanyakazi wa mashirika ya misaada uhakikishwe, na wale wenye uhitahaji waweze kuhama kwa usalama.

Wakati huo huo, Israel imesema usitishaji mapigano utaanza kutekelezwa ndani ya saa 24 baada ya mkutano wa baraza la mawaziri la usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *