Katika maoni yake yaliyochapishwa Alhamisi na vyombo vya habari, Zelensky amesema kazi ya Urusi ni kuleta machafuko na kuweka shinikizo la matatizo ya kisaikolojia kwa watu kupitia mashambulizi katika miundombinu ya reli na nishati.

”Mashambulizi ya Urusi kwa mwaka huu tayari yameiweka miundombinu ya gesi ya Ukraine chini ya shinikizo kubwa,” alifafanua Zelensky.

Bei ya gesi kutopanda

Aidha, Zelensky amesema watahakikisha wanaweka bei maalum ya gesi kwa watumiaji wa nyumbani wakati wa msimu huu wa baridi na kwamba hawatopandisha bei ya gesi.

Kulingana na kiongozi huyo wa Ukraine, mashambulizi zaidi katika miundombinu ya gesi na reli yanaweza kuilazimisha nchi hiyo kuongeza uagizaji wa nishati kutoka nje.

Hivi karibuni, Ukraine imeongeza pia mashambulizi ya droni na makombora kwenye ardhi ya Urusi katika operesheni ambazo Zelensky amesema zinaonesha matokeo, na ambayo yameongeza bei ya mafuta nchini Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *